Eastern Africa Journal of Kiswahili
https://www.ajol.info/index.php/eajk

Eastern Africa Journal of Kiswahili (ISSN 2958-1036) is a double-blind peer reviewed, open access, online Journal published by Editon Consortium Publishing, East Africa, Kenya. The Journal publishes original scholarly research (empirical and theoretical), in form of case studies, reviews and analyses in Kiswahili Linguistic Studies.

Aims and Scopes

The Journal publishes original scholarly research (empirical and theoretical), in form of case studies, reviews and analyses in Kiswahili Linguistic Studies.

You can see the journal's own website here.

Editon Consortium Publishing Website-https://editononline.com/ Mailing address: info@editononline.com
en-US
Eastern Africa Journal of Kiswahili
2958-1036

Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/328834

Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Riwaya hizo ni Tumaini (2006) ya Clara Momanyi, Dago wa Munje (2008) ya Sheila Ryanga, Kipimo cha Mizani (2004) ya Zainabu Burhani, na Hiba ya Wivu (1997) ya Zainabu Mwanga. Kuna dhamira za uchapakazi, ndoa, maadili, umuhimu wa elimu, malezi na migogoro ingawa makala hii imejikita katika dhamira mbili ambazo zinalinganishwa katika riwaya teule. Riwaya hizi nne zimeteuliwa kimakusudi kulingana na maudhui mazito yaliyomo katika riwaya hizo kuhusu wanaume. Makala hii imeonesha kuwa nadharia ya ujifunzaji wa kijamii (imejikita kwenye uana) na mwanaume mpya zimekuwa nadharia faafu katika makala hii. Nadharia ya ujifunzaji wa kijamii huona tabia kama kitendo ambacho mtu hujifunza kutoka katika mazingira ambayo ndiyo hupelekea umuhimu wa majukumu ya kiana. Mwisho, makala hii imetumia nadharia ya mwanaume mpya, nadharia inayojaribu kuelezea kwanini baadhi ya wanaume hukaa na wake zao kwa usawa bila tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume. Mbinu ya Fasihi Linganishi imetumika kulinganisha usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya teule kupitia dhamira wanazowasilisha. Data iliyotumika katika Makala hii ilitolewa maktabani kwa kusoma tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo. Matokeo yameonesha kuwa waandishi wa kike wamemsawiri mwanamume kwa mtazamo chanya zaidi kuliko hasi. Kwa hiyo, kulingana na waandishi wa kike wa Tanzania na Kenya wameonesha kuwa mwanamume ni mpya kulingana na mpito wa wakati ambapo mambo mbalimbali ya ugandamizaji wa kijinsia yametupiliwa mbali ili kuleta uwiano wa kiana.

Olivia Kanwa
Catherine Ndungo
Richard Wafula
Copyright (c) 2026
https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0
2026-06-30
2026-06-30
5 1
1
10

Mchango wa Miktadha ya Kijamii katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili Nchini Burundi
https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/328836

Makala hii inahusu miktadha ya kijamii na mchango wake katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya pili nchini Burundi. Utafiti huu ulifanyika Nchini Burundi, Mkoa wa Bujumbura, katika Tarafa za Mukaza na Ntahangwa. Kimahususi zaidi utafiti huu ulifanyika katika vyuo vikuu vya serikali ambavyo vina idara za Kiswahili yaani Chuo Kikuu cha Ualimu (ENS) na Chuo Kikuu cha Burundi (UB). Nadharia ya Mwingiliano Jamii iliyoasisiwa na Mwanasaikolojia Vygotsky (1978) iliongoza utafiti huu. Utafiti huu ulitumia sampuli ya wasailiwa ishirini (20) wa kiwango cha shahada ya awali, mwaka wa tatu. Sampuli tajwa ilipatikana kwa usampulishajinasibu sahili. Ukusanyaji wa data uliwezeshwa na mbinu ya usaili. Mikabala ya kitaamuli na kitakwimu na mbinu ya uchanganuzi wa data kimaelezo imetumika katika uchanganuzi wa data za utafiti huu. Data za utafiti huu zimewasilishwa kwa kutumia majedwali na grafu zilizoambatana na maelezo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi zaidi. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa miktadha ya kijamii ya kujifunza Kiswahili jijini Bujumbura ni soko, hospitali, zahanati, nyumbani, na kadhalika. Matokeo pia yalionesha kuwa miktadha hiyo inawawezesha wanafunzi kuingiza msamiati mpya, kukuza stadi za kusikiliza na kuzungumza. Inawawezesha pia, kuimarisha umilisi wa utamaduni na maarifa kuhusu fasihi. Mwisho, makala hii inapendekeza serikali ya Burundi iwezeshe walimu wa Kiswahili kufuatilia ujifunzaji wa Kiswahili wa wanafunzi nje ya darasa.

Consolée Kamaro
Rajabu Chipila
Copyright (c) 2026
https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0
2026-06-30
2026-06-30
5 1
11
23

Uchanganuzi wa Majina ya Wanaume Katika Jamii ya Watugen
https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/328837

Utafiti huu ulichambua majina ya wanaume katika jamii ya Watugen, Kaunti ya Baringo ya Kati, Kenya. Lengo kuu lilikuwa kuchunguza majina haya miongoni mwa wanajamii wa eneo hilo. Ingawa majina ya kipekee katika jamii hii hujumuisha yale yanayotokana na mito, milima, vijiji, miji, watu na nchi, uchunguzi ulijikita kwenye majina ya wanaume pekee. Makala hii inajumuisha vijisehemu vifuatavyo: maelezo mafupi kuhusu jamii ya Watugen, utamaduni wa kupeana majina, sherehe zinazohusiana na kupeana majina, majina ya wanaume pamoja na maana zao, na hitimisho. Utafiti uliongozwa na nadharia ya simiotiki, ambayo inasisitiza kuwa kila ishara ina maana yake maalum. Data zilikusanywa kwa njia ya uchunguzi wa nyanjani kwa kutumia mbinu ya mahojiano. Washiriki 50, ambao walikuwa watu wazima wenye umri kati ya miaka 35 na 70, walihojiwa kwa muda wa majuma mawili. Sampuli ya majina iliorodheshwa katika majedwali ili kuwezesha uchambuzi. Utafiti uliongozwa na maswali yanayohusu Watugen ni watu wa wapi, sherehe zipi zilihusiana na kupeana majina, sababu za ujinaishaji zilikuwa zipi, kategoria zipi za majina zilikuwepo, na maana za majina ya wanaume zilikuwa zipi. Majibu ya maswali haya yaliunda kiini cha utafiti. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa majina ya wanaume yalitokana na hali halisi za kijamii katika jamii ya Watugen, na kila jina likibeba maana maalum. Ilibainika kuwa ujio wa wageni, hasa wamishonari, uliathiri sana mchakato wa ujinaishaji. Zaidi ya hayo, majina hayo yana miundo mbalimbali.

Dave Bowen
Copyright (c) 2026
https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0
2026-06-30
2026-06-30
5 1
24
31

Tamthilia za Kiswahili kama Chombo cha Uhamasishaji kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu: Mifano ya Mwinyi na Manyani ya Adili na Kodi
https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/328838

Azma ya makala hii ni kuchunguza tamthilia za Kiswahili kama chombo cha kuhamasisha jamii kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (MME). MME ni mpango ulioidhinishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2015 na umekumbatiwa na serikali, mashirika na wasomi mbalimbali duniani.Utafiti huu ni wa kithamano na unaongozwa na Nadharia ya Uhistoria Mpya iliyoasisiwa na Stephen Greenblatt (1980) na kuendelezwa na Brizee na Tompkins (2012). Muundo wa kiuchambuzi ulitumika kuchunguza jinsi tamthilia teule zinavyoakisi na kuhoji masuala ya kijamii yanayohusiana na MME. Data ilikusanywa kwa mbinu ya unukuzi wa madondoo mahususi kutoka katika tamthilia teule kwa kutumia usampulishaji wa kimaksudi.Tamthilia zilizochaguliwa ni Mwinyi na Manyani ya Adili (Mbogo, 2022) na Kodi (Muhando, 2024) kwa sababu zinaangazia masuala ya MME na ziliandikwa kati ya mwaka 2016 na 2026, yaani kipindi cha utekelezaji wa malengo hayo. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo ya maandishi. Utafiti umebaini kuwa tamthilia hizi zinahamasisha kwa kiasi kikubwa malengo yafuatayo: L1 (kutokomeza umaskini), L2 (kutokomeza njaa), L5 (usawa wa kijinsia), L8 (ajira na ukuaji wa uchumi), L11 (miji na makazi endelevu) na L16 (amani, haki na taasisi imara). Masuala haya yanajitokeza kupitia wahusika, migogoro na maamuzi yao. Hata hivyo, malengo mengine kama L3 (afya bora), L4 (elimu bora), L6 (maji safi na usafi wa mazingira), L7, L9, L10, L12, L13, L14 na L15 hayajaangaziwa vya kutosha au yamepuuzwa kabisa. Makala hii inapendekeza kwamba waandishi wa tamthilia za Kiswahili wanapaswa kupanua wigo wa maudhui yao kwa kujumuisha kimaksudi malengo yaliyopuuzwa, hasa L3, L4 na L6, ili kuimarisha mchango wa fasihi katika uhamasishaji mpana wa MME.

Ogonda Samuel Sinzore
Copyright (c) 2026
https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0
2026-06-30
2026-06-30
5 1
32
41

Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/328840

Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi wa kufana hujengeka kwa tamaduni zinazokubalika na zenye kuheshimika. Makala haya yalipambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Malengo mahususi yalikuwa ni: Kutathmini utamaduni wa uongozi wa shule; kubainisha ni jinsi gani Kiswahili kinatumika kujenga utamaduni wa uongozi wa shule; na kupambanua mitazamo ya washikadau kuhusu matumizi ya Kiswahili katika uongozi wa Shule ya Msingi ya Mungakha. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Tabia ya Uongozi ya Fleenor (2006). Mkabala wa kithamano na muundo wa kimfano uliongoza utafiti huu. Mbinu ya ukusanyaji wa data iliyotumiwa ni hojaji. Sampuli lengwa ilihusisha shule moja ya msingi, mwalimu mkuu, naibu wake, wakuu wa jopo, viranja, wanachama wa halmashauri ya uongozi wa shule, wafanyakazi na wazazi. Usampulishaji wa kimaksudi uliteua Shule ya Msingi ya Mungakha, mwalimu mkuu na naibu wake. Usampulishaji wa kinasibu uliwachagua wanachama wa halmashauri ya usimamizi wa shule, wakuu wa jopo, viranja na wafanyakazi. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia kielelezo cha nyaraka, kisha ikawasilishwa kwa kurejelea malengo ya utafiti kwa maelezo ya kifafanuzi na mijadala kutolewa. Matokeo yalibainisha kuwa utamaduni katika Shule ya Msingi ya Mungakha ulikuwa wa umoja, uongozi wa kielelezo, mazingira bora ya ujifunzaji, ugatuzi wa mamlaka, kushirikishwa kwa wanafunzi, kuhusishwa kwa wazazi na mawasiliano ya wazi. Lugha ya Kiswahili na Kiingereza zilitumika kwa kiwango kizuri huku Kinyala kikitumika kwa kiwango cha chini. Washikadau walipendelea matumizi ya lugha yaKiswahili na Kiingereza kwa kiwango cha wastani na Kinyala kwa kiwango cha chini sana katika shule hii.

Stephen Muyundo Ndinyo
Ernest Sangai Mohochi
Copyright (c) 2026
https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0
2026-06-30
2026-06-30
5 1
42
53

Maana Kisemiotiki Na Kipragmatiki Za Ujumbe Katika Mabango Ya Afya
https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/328841

Makala hii inalenga kuchanganua maana kisemiotiki na kipragmatiki ya jumbe kwenye mabango ya afya. Licha ya matumizi yake katika mawasiliano ya umma, bado kuna changamoto katika uelewa wa kina wa jinsi maana zinavyoundwa na kufasiriwa. Utafiti ulichunguza kwa kina miundo ya ishara inayotumika kwenye mabango ya afya na mchango wa muktadha katika uundaji wa maana. Mabango yalitokana na vituo vya afya vya kiwango cha pili vya serikali. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Uhusiano iliyoasisiwa na Sperber na Wilson (1986) na kuendelezwa na Clark (1996) pamoja na Nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Saussure (1916) na kuendelezwa na Peirce (1931-1958). Nadharia ya Uhusiano ilitumika kueleza jinsi maana zilivyofasiriwa kwa kuzingatia muktadha, huku nadharia ya semiotiki ikitumika kuchanganua ishara. Muundo wa utafiti ulikuwa wa kiuchanganuzi kwa kutumia data za kithamano. Usampulishaji ulikuwa kimakusudi kwa mabango yaliyoandikwa kwa Kiswahili katika vituo hivyo. Data zilikusanywa kwa usomaji wa kina wa nyaraka na mabango, na kuchanganuliwa kwa mbinu ya uchambuzi wa yaliyomo. Matokeo yalionyesha kuwa rangi zilitumika kisemiotiki kuwasilisha taarifa mbalimbali, huku picha zikiimarisha ujumbe. Kipragmatiki, maana ya ujumbe ilitegemea muktadha. Msamiati ulipata maana mpya kulingana na muktadha wa matumizi. Rangi na picha vilitumika kimakusudi kuimarisha maana ya jumbe. Utafiti unahitimisha kwamba wabunifu wa mabango wanapaswa kutumia rangi na ishara wakizingatia maana yake kisemiotiki na kitamaduni. Matokeo yanatarajiwa kuwasaidia wabunifu wa mabango ya afya na wataalamu wa mawasiliano kuimarisha sera na mipango ya afya ya umma.

Alice Khayali Mukoko
Fridah Miruka
Deborah Amukowa
Copyright (c) 2026
https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0
2026-06-30
2026-06-30
5 1
54
64

Mageuzi ya Kimofolojia ya Msamiati wa Mame-Bantu kwenda Lugha za Kibantu: Mifano kutoka Kinyakyusa
https://www.ajol.info/index.php/eajk/article/view/328842

Makala hii inahusu mageuzi ya kimofolojia kutoka Mame-Bantu (MB) kwenda Kinyakyusa. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza mabadiliko ya kimofolojia ya maumbo ya vitenzi na nomino kutoka MB kwenda lugha ya Kibantu. Utafiti huu ni wa kitaamuli na uliongozwa na Nadharia ya Mofolojia Asilia ya Wolfgung U Dressler (1987). Data za utafiti zilikusanywa kwa njia ya uchambuzi wa matini pamoja na usaili wa wazungumzaji asilia wa Kinyakyusa. Jumla ya maumbo ya msamiati 35 ya MB yalichambuliwa kutoka kwenye matini ya Bostoen na Bastin (2016), kisha kufasiriwa kwa Kinyakyusa. Aidha, usaili uliofanyika kwa wazungumzaji asilia sita (06) wa Kinyakyusa ulilenga kupata tafsiri ya maumbo ya vitenzi na nomino zilizochunguzwa. Sampuli ya utafiti iliteuliwa kwa kutumia usampulishaji lengwa wa kipekee na kwa kuzingatia vigezo vya umri, jinsi na umahiri wa lugha. Matokeo ya utafiti yalionesha kuwapo kwa mageuzi ya kimofolojia ya msamiati wa MB kwenda Kinyakyusa. Mageuzi haya yanachagizwa na mabadiliko ya vitamkwa kama vile vipasuo kuwa vipasuo kwamizi kupitia uyeyushaji wa irabu. Pia, kipasuo kuwa likwidi au sauti za likwidi kutokana na uimarishaji au udhoofishaji wa konsonanti. Vilevile, uchunguzi ulibaini kuwapo kwa mageuzi si-kamilifu ambayo huhifadhi umbo asilia la mzizi wa neno la MB katika lugha ya Kinyakyusa. Pia kulibainika kuwapo kwa mageuzi kamilifu ya kimofolojia ambayo hayahifadhi umbo asilia la msamiati wa MB katika lugha za Kibantu. Kwa kuwa utafiti huu ulijikita katika umbo la msamiati pekee, tafiti zingine zijazo zinaweza kuchunguza kuhusu mageuzi na/au uhifadhi wa maana kupitia toni na miundo ya tungo kutoka Mame-Bantu kwenda lugha nyingine za Kibantu, kikiwamo Kiswahili.

Emanuel Deogratius
Copyright (c) 2026
https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0
2026-06-30
2026-06-30
5 1
65
78