Main Article Content

Tafsiri ya Mazungumzo Katika Filamu za Kiswahili


H Pembe

Abstract

Taaluma ya tafsiri huingiliana na nyanja nyingine za kitaaluma kutokana na kujishughulisha kwake katika mawasiliano. Makala haya yanachunguza tafsiri ya mazungumzo ya Kiingereza katika filamu za Kiswahili nchini Tanzania. Filamu zilizoteuliwa katika uchunguzi ni ile ya Vita Baridi na Love & Power. Kimahususi, makala imechunguza mikakati mbalimbali iliyotumika kupata tafsiri ya mazungumzo ya Kiingereza kwenye filamu za Kiswahili wakati inajulikana kwamba mfumo wa mazungumzo na maandishi hutofautiana kisifa. Pia tafsiri ya mazungumzo ina kanuni na sheria zake. Sambamba na hayo, lugha ya Kiswahili na Kiingereza hutofautiana kiisimu, kitamaduni, kimazingira pamoja na kihistoria. Data zimechambuliwa kwa kuongozwa na nadharia ya ulinganifu kama ilivyoasisiwa na Nida na kisha kuendelezwa na Catford na Newmark. Makala imebaini kwamba
matini asilia humwongoza mtafsiri kutumia mikakati kama vile udondoshaji, ufupishaji, ufafanuzi kimuhtasari, uingizaji na matumizi ya tarakimu katika mchakato wa tafsiri ya mazunugmzo ya Kiingereza kwenye filamu za Kiswahili.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-6739