Uainishaji wa kategoria ya kihusishi katika lugha ya Kiswahili

  • Fokas Mkilima

Abstract

Kategoria ya kihusishi katika lugha ya Kiswahili imeonekana kuwa na mkanganyiko katika uainishaji wake. Wanaisimu wameonekana kutofautiana kuhusu uainishaji wa kategoria hii. Baadhi ya wanaisimu wamekuwa wakiweka maneno ya kategoria ya kihusishi katika kategoria ya viwakilishi, vivumishi na viunganishi. Kutokana na mkanganyiko wa yapi ni maneno yanayoingia katika kategoria ya vihusishi, makala hii inabainisha maneno ya kategoria ya vihusishi ili kupunguza au kuondoa mkanganyiko juu ya kategoria ya vihusishi katika lugha ya Kiswahili. Utafiti huu ulitumia mbinu ya uchanganuzi wa nyaraka kutoka katika maandiko ya wanaisimu wa lugha za kigeni pamoja na wa Kiswahili. Uchanganuzi huo ulizingatia uainishaji wa kategoria ya vihusishi, aina za vihusishi, fasili, sifa na dhima ya vihusishi. Pia, mtazamo wa kisasa umetumika katika kubainisha kategoria ya vihusishi. Mtazamo huu unatumia kigezo cha kisintaksia katika kuainisha maneno kwa kuzingatia mtawanyiko wake, dhima kisarufi na mnyambuliko wa aina hii ya maneno. Vilevile, kigezo cha kimofolojia na kisemantiki kimetumika. Makala hii inatumia vigezo hivyo katika kubainisha kategoria ya vihusishi katika lugha ya Kiswahili.

Published
2021-09-07
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789