Main Article Content

Nyimbo za taifa na Jumuiya na utambulisho wa jamii


Method Samwel

Abstract

Wataalamu wa fasihi, utamaduni, muziki, anthrolopolojia na siasa wamekuwa wakizitazama nyimbo za taifa na jumuiya kama alama za utaifa na ujumuiya. Huzitazama kama nyenzo za kueleza tamaduni za taifa na jumuiya husika na kuleta umoja. Pia, huzitazama kuwa ni utambulisho wa taifa au jumuiya husika. Hata hivyo, uhakiki wetu wa nyimbo za Kiswahili za taifa na jumuiya umebainisha kuwa mtazamo huo una walakini. Hivyo, makala hii inabainisha maeneo mbalimbali yenye dosari katika wimbo wa taifa wa Tanzania, Kenya na wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Inaonesha kuwa dosari hizo zinazifanya nyimbo husika kushindwa kuwa utambulisho wa kweli wa taifa na jumuiya husika. Ili kubainisha hayo, makala hii inatumia Nadharia ya Utambulisho wa Kijamii ya Tajfel na Turner. Aidha, makala hii inatokana na utafiti wa kitaamuli uliohusisha ushuhudiaji, mahojiano na udurusu na uchambuzi matini.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789