Main Article Content

Maneno ya Heshima katika Kiswahili: Utendi wa Wazungumzaji Wazawa Kulingana na Rika na Jinsi zao Mjini Zanzibar


Hassan G. Haji

Abstract

Wazungumzaji wazawa wa Kiswahili wa Zanzibar wana dasturi zao katika kuitana. Kabla ya jina hutanguliza neno la heshima. Hali hii hutokea kwa wakubwa na wadogo, wanaojuana na wasiojuana. Makala haya yanahusu maneno ya heshima (onorafiki) katika Kiswahili, namna yanavyotumiwa na wazungumzaji wazawa kulingana na rika na jinsi zao. Makala hasa yanazungumzia namna wazungumzaji wazawa wa lugha ya Kiswahili wa Zanzibar wanavyotumia maneno ya heshima katika kuitana katika mazungumzo yao ya kila siku katika nyumba na maskani zao za mazungumzo na katika sehemu zao mbalimbali za kazi. Data ya utafiti huu imeonesha kuwa maneno ya heshima yanatumika kulingana na rika za watu. Aidha, data imeonesha kuwa wazawa wa lugha ya Kiswahili huyatumia maneno ya heshima katika kuonesha uhusiano wa kifamilia na uhusiano usiokuwa wa kifamilia ili kujenga usuhuba na heshima katika mazungumzo. Wazawa wa lugha ya Kiswahili huelimishana kuitana na kuyatumia maneno ya heshima tangu wanapokuwa wadogo kama data inavyoonesha kuwa mzazi anaweza kumwita mtoto wake baba au mama, bibi au babu, mjomba au shangazi na kadhalika.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X