Main Article Content

Kufungamana kwa Fasihi Simulizi na Riwaya ya Kiswahili ya Kimajaribio: Uchambuzi wa Visasili katika <i>Bina-Adamu</i>


Joviet Bulaya
Aswile Mkumbwa

Abstract

Lengo la makala haya ni kutalii sababu zinazomfanya mwandishi wa riwaya ya Kiswahili ya Kimajaribio kutumia mbinu mbalimbali za kifasihi simulizi kama vile visasili katika uandishi wake. Ni dhahiri kuwa dhima ya masimulizi ya visasili na mbinu zake za uwasilishaji zinachukua nafasi kubwa katika riwaya ya Kiswahili ya Kimajaribio. Maswali yanayoweka msingi wa mjadala katika makala haya ni: Kwa nini waandishi wa riwaya ya Kiswahili ya Kimajaribio huingiza masimulizi ya visasili katika riwaya zao? Je, visasili hivyo huwa na dhima gani kwa mwandishi na msomaji wa riwaya inayohusika? Makala haya yanajaribu kuyajibu maswali haya kwa kurejelea riwaya ya Bina-Adamu ya Wamitila (2002a).

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X