Main Article Content

Maudhui ya Kihalisia katika Riwaya Dhahania za Katama Mkangi: Mfano wa <i>Walenisi</i> na <i>Mafuta</i>


Matthew Kwambai
Furaha Chai
Wendo Nabea

Abstract

Makala hii inatathmini suala la uhalisia katika riwaya za Katama Mkangi hasa unavyodhihirika kupitia maudhui. Uhalisia katika fasihi ni kigezo ambacho humsaidia mtunzi kuangaza mambo kama yalivyo katika jamii. Hata hivyo, riwaya za Walenisi na Mafuta, sawa na riwaya nyingi mpya za Kiswahili, zinajenga uhalisia wake katika misingi ya udhahania. Ujenzi huu unazua mushkeli ikizingatiwa kuwa riwaya asisi ya Kiswahili ilipigwa vita na baadhi ya wahakiki kwa kujikita katika udhahania; tofauti na riwaya za miaka ya 1970 na 1980 ambazo zilishamiri uhalisia. Lakini riwaya za miaka ya 1990 hadi leo zimechanganya uhalisia na mazingaombwe suala ambalo linazua kizungumkuti iwapo uhalisia unaweza kujengeka katika udhahania. Makala hii kwa kuegemea nadharia ya usasaleo inabaini kuwa matumizi ya udhahania ni kigezo cha kuwadhihirishia wanajamii mazingaombwe yanayotumiwa na watawala kuwapumbaza wananchi ili waendelee kukubali hali yao duni huku wachache walio uongozini wakinufaika. Hatimaye, makala hii inadhihirisha kuwa japo riwaya za Katama Mkangi zimejengeka katika udhahania, bado zina uyakinifu mwingi katika jamii za Kiafrika za hivi leo.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X