Main Article Content

Tofauti baina ya Vivumishi na Vibainishi katika Lugha ya Kiswahili


Zabron T. Philipo

Abstract

Nia ya makala hii ni kuonyesha tofauti ya dhana ‘kivumishi’ na ‘kibainishi’ katika lugha ya Kiswahili. Wanaisimu wengi, kwa kutumia mtazamo wa kimapokeo, wamekuwa wakichanganya dhana hizi mbili katika lugha hii ambapo vibainishi vimekuwa vikiwekwa kwenye ‘kapu’ moja na vivumishi. Kutokana na kuwapo kwa utata huo, makala hii inazitalii dhana hizi mbili ili kujaribu kuondoa au kupunguza utata unaowakabili wanaisimu katika kuzipambanua dhana hizi katika lugha ya Kiswahili. Mbinu ya udurusu wa nyaraka ilitumika kupata data za makala hii1. Mtazamo wa kisasa katika kuainisha tofauti baina ya vivumishi na vibainishi ulitumika. Mtazamo huu unasisitiza kutumia kigezo cha kisintaksia kupambanua aina hizi za maneno kwa kuzingatia: mosi, mtawanyiko wake, pili, dhima kisarufi, na tatu, mnyambuliko wa aina hizi za maneno. Aidha, makala hii inapendekeza vigezo na namna nyingine za kuainisha vibainishi na vivumishi katika lugha ya Kiswahili.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X