Main Article Content

Uelekeo wa Maana za Kipolisemia katika Msamiati wa Kiswahili: Mifano kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu


Faraja J. Mwendamseke

Abstract

Vipengele mbalimbali vya sarufi vinapopitia michakato ya mabadiliko vina uelekeo fulani. Pia, maana za maneno na tungo hukumbwa na mabadiliko mbalimbali. Mabadiliko ya maana za maneno huweza kutokea katika visawe na polisemia. Ullmann (1967) anaeleza kuwa polisemia ni sifa ya msingi katika mazungumzo ya binadamu ambapo licha ya kuwa na maana zaidi ya moja, maana hizo huwa zina uhusiano. Pia anaeleza kuwa kwa kiasi kikubwa polisemia hutokana na uhamishaji wa matumizi ya neno hilo kutegemeana na lugha inayohusika. Maelezo haya yanadokeza kuwa kuna uelekeo fulani wa mabadiliko ya maana katika polisemia. Katika makala hii tumechunguza uelekeo wa mabadiliko ya maana za kipolisemia katika lugha ya Kiswahili ili kueleza utokeaji wake na namna zinavyobainishwa katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu na changamoto zinazoweza kujitokeza katika ubainishaji huo. Data iliyotumika ni kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI, 2013). Ili kukidhi malengo hayo tumetumia Nadharia ya Maana kama Dhana, ambapo tunahusisha maana (dhana) mpya za kipolisemia na maana ya msingi ya neno hilo. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa polisemia huwa na maana zaidi ya moja zinazohusishwa na fikra/wazo moja (maana ya msingi) na, utokeaji wake upo wa aina tofauti. Aina hizo; ni uhamishaji wa matumizi, ufananisho wa kisitiari, uwanja maalum katika jamii na kuwapo kwa maneno yenye asili ya kigeni. Kuna wakati utokeaji huu hutegemeana na aina ya neno husika kama ni nomino au kitenzi. Masuala haya hujibainisha wazi katika kamusi. Hata hivyo kuna baadhi ya changamoto zinajitokeza polisemia zinapobainishwa katika kamusi.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X