Main Article Content

Kiswahili katika karne ya 20 : chombo cha ukombozi, utaifa na ukandamizaji


Jean de Dieu Karangwa

Abstract

Historia ya Kiswahili katika karne ya 20 ni mada ambayo imechunguzwa na watafiti kadhaa katika miaka iliyopita. Orodha yao ikiwa ndefu, tutataja wachache miongoni mwao kama vile Whiteley (1969), Heine (1970), Chiraghdin na Mnyampala (1977), Polome (1982), Fabian (1986), Mbaabu (1991), Legere (1992), Karangwa (1995)… Bila kurudia mambo ambayo wamezungumzia tayari na tena vizuri, makala hii ina nia ya kuleta mwanga pale itakapotakiwa na kuonyesha:
(i) Jinsi historia ya watu wanaozungumza Kiswahili ilivyoathiri historia ya lugha hiyo
(ii) dhima ya lugha hiyo katika nyanja mbalimbali za maisha ya Waswahili na, yaani wale wote wanaozungumza Kiswahili barani Afrika, bila kusahau hadhi yake, dhana hizo mbili zikiingiliana na kutegemeana kwa namna fulani.
Mkazo utatiliwa hasa sehemu Kiswahili kilipoenea mwisho yaani Afrika ya kati. Upwa wa Afrika Mashariki umezungumziwa ya kutosha na ukitajwa itakuwa kama kweli ni muhimu.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X