Main Article Content

MATATIZO YA KUTUMIA KIINGEREZA KUFUNDISHIA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI NA VYUO VYA JUU TANZANIA


M.A.S Qorro

Abstract

Makala hii inaeleza matatizo yanayotokana na kutumia Kiingereza kufundishia katika shule za sekondari na vyuo. Makala inaanza kwa kufafanua tofauti zilizopo kati ya kufundisha lugha kama somo kwa lengo la kupanua mawanda ya mawasiliano na kutumia lugha kama nyezo ya kutolea maarifa. Makala imebainisha matatizo ya kijamii, kiutamaduni, kiuchumi, kielimu na kiakili yanayotokana na kutumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia. Katika kubainisha matatizo hayo; makala imetumia vielelezo mbalimbali kutoka kwa walengwa wa viwango tofauti vya elimu; kuanzia kidato cha kwanza hadi chuo kikuu. Makala inahitimisha kwa kupendekeza kuwa ni vema kutumia lugha inayoeleweka; lugha ya Kiswahili, ili wanafunzi waweze kupata maarifa, kisha kutafuta mbinu za kufundisha lugha ya Kiingereza kama somo kwa ufasaha zaidi ili itusaidie katika mambo mbalimbali.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X