Main Article Content

KISWAHILI KWA KUFUNDISHIA: SERA NA MIKAKATI


Y.S.M Mochiwa

Abstract

Makala haya yanajadili matatizo ya lugha ya kufundishia katika shule za sekondari na vyuo. Makala yanaeleza kuwa matatizo wanayopata wanafunzi yanatokana na ukosefu wa msingi imara wa sarurufi ya lugha ya Kiingereza, ambayo hutumiwa kufundishia. Hali hii inawafanya wanafunzi kukosa stadi za kufikiri, kutambua na kuchambua mambo wanayojifunza kwa uhakika. Aidha, makala yanasisitiza kuwa kuna haja ya kubadili sera ya elimu ili kunusuru hali hii.

Pia, makala yanaeleza mambo muhimu katika utekelezaji wa sera mpya ya elimu. Baadhi ya mambo hayo ni: tamko rasmi la kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia sekondari na vyuo, uimarishaji wa ufundishaji wa lugha ya Kiingereza, uandaaji wa mitaala na uandaaji wa semina mbalimbali zitakazotoa msingi kwa walimu wa lugha ya Kiswahili.

Makala yanahitimisha kwa kueleza kuwa, utekelezaji wa sera mpya una mambo yafuatayo ambayo ni muhimu; tamko la sera, ushiriki wa wanajamii katika kutumia lugha, vyombo vya ukuzaji lugha pamoja na wataalam wa lugha.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X