Main Article Content

ULINGANISHI WA MUUNDO WA VITOMEO KATIKA KAMUSI MBILI ZA KISWAHILI - KIINGEREZA


E.K.F Chiduo

Abstract

Ulinganishi wa Kamusi Sanifu ya Kiswahili-Kiingereza (KSKK, 1993) na Kamusi ya Kiswahili- Kiingereza (KKK, TUKI 2001) unazingatia mtazamo wa Nkweti-Azel. Mtizamo huu unazingatia vipengelele vikuu vinane vilivyogawanyika katika vipengele vidogo 21:
(i) Otografia ( Kitomeo, kibadala, kisawe)
(ii) Fonolojia (matamshi)
(iii) Mofolojia na Sintaksia ( viambiasi wingi, ngeli za nomino, vinyambuo, uelekezi)
(iv) Kategoria za maneno
(v) Pragmantiki (tahadharia ya matumizi alama za rejesta za kijiografia)
(vi) Etimolojia (asili, maneno husiani)
(vii) Fasiri ( fasiri ya maneno, mifano muktadha)
(viii) Uhusiano (Kinyume, maneno husiani)

Ulinganishi huu unaonesha kuwa, KSKK iliingiza vipengele vidogo 14 na kuacha 7 wakati KKK iliingiza vipengele vidogo 12 na kuacha 9. Ni KKK tu iliyoingiza taarifa za ngeli za nomino na uelekezi.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X