Main Article Content

Usawiri wa Mwanamke katika Nyimbo za Kizazi Kipya


SE Mrikaria

Abstract

Makala haya yanachambua usawiri wa mwanamke katika baadhi ya kazi za wasanii wa nyimbo za kizazi kipya nchini Tanzania. Mwanamke anasawiriwa kupitia nyimbo za Kiswahili za muziki wa dansi, taarabu, dini na hata Kizazi Kipya kila wakati. Ili kushuhudia namna mwanamke alivyosawiriwa na wasanii wa nyimbo za Kizazi kipya, tunawarejelea wasanii wachache wa nyimbo hizo ili kushadidia kile kinachozungumzwa kuhusu taswira ya mwanamke katika jamii inayomzunguka. Makala yanaegemea katika nadharia ya ufeministi, hususan ufeministi wa Kiafrika, ambapo matatizo ya udhalilishwaji, ukandamizwaji na udunishwaji wa mwanamke wa Kiafrika yanaangaliwa. Makala yanaanza kwa utangulizi ambapo usuli wa uhusika wa wanawake unaelezwa na kubainishwa. Makala yanaangalia kwa ufupi dhana ya mwanamke katika jamii, na kuelezea nafasi ya mwanamke katika nyimbo za Kiswahili za kizazi kipya. Mwishoni mwa makala haya kuna hitimisho linalotoa majumuisho ya mjadala.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X