Main Article Content

“Bongo Fleva Inapotosha Jamii”: Je, ni Dai Jipya katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili?


M Samwel

Abstract

Muziki wa Bongo Fleva umepitia kipindi kigumu cha kihistoria kwa kukataliwa na kuonekana kwa unapotosha jamii. Japo kwa sasa muziki huu unaonekana kukubalika, bado kuna baadhi ya watu wanauona kwamba unapotosha jamii. Miongoni mwa mambo yaliyoufanya muziki huu ukataliwe na kuhusishwa na upotoshaji wa jamii ni mavazi ya wasanii wake, maneno ya kihuni yanayotumika, tabia za wasanii, matumizi ya madawa ya kulevya, pombe na mengine ya aina hiyo. Makala haya yanapitia na kuangalia ikiwa dai kwamba kazi za fasihi hasa muziki wa Bongo Fleva unapotosha jamii ni jipya au la. Aidha, makala haya yanatoa mwelekeo mpya wa kufuatwa na wanajamii katika kuzihukumu kazi za fasihi za aina hiyo.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X