Main Article Content

Filamu za Kiswahili nchini Tanzania: Athari za ‘Kauli’ za Wasambazaji-Wauzaji kwa Wasanii na Jamii


Vicensia Shule

Abstract

Baadhi ya tafiti zilizofanyika katika tasnia ya filamu za video (filamu) za Kiswahili nchini Tanzania zimeonesha kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya utayarishaji filamu na uuzaji wake. Uhusiano huo ni ule unaoonesha jinsi mchakato wa utayarishaji filamu unavyoweza kuathiri ubora wa filamu, hususan ukosefu wa elimu na taaluma ya filamu kwa wasanii. Pamoja na hayo, tafiti hizo hazikuweza kuweka bayana namna usambazaji unavyoweza kuathiri ubora wa filamu. Makala haya yanalenga kujenga hoja kuwa ubora wa filamu Tanzania ni suala linalochangamana zaidi na mfumo wa usambazaji na uuzaji wa filamu kuliko utayarishaji. Lengo hasa ni kuonesha jinsi ambavyo ubora wa filamu za Tanzania unavyopangwa na wasambazaji-wauzaji na siyo warudufishaji-wasambazaji au wasanii-watayarishaji kama inavyoonekana katika tafiti zilizotangulia. Kauli mbalimbali za wadau hao ndizo tunazozichanganua katika makala haya.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X