Main Article Content

Kufasiri, Kukalimani na Kurudufu Matini kwa Lugha Nyingine: Tulikotoka hadi Tulipo Sasa


Titus Mpemba

Abstract

Umuhimu wa tafsiri na ukalimani katika mawasiliano umeongezeka kutokana na utandawazi ambao umerahisisha utangamano na mawasiliano ya watu wazungumzao lugha tofauti. Pamoja na umuhimu huu, bado baadhi ya watu hawajaelewa sawasawa namna kazi za wafasiri na wakalimani zinavyofanyika. Hivyo, wanajikanganya na kudai kuwa kufasiri au kukalimani si lolote, bali ni kurudia tu yaliyosemwa au kuandikwa na mtu mwingine kwa lugha nyingine. Hata hivyo, wapo wanaoona kuwa tafsiri au ukalimani ni zaidi ya kurudufu matini chanzi kwa lugha nyingine kwani ni sanaa na ni sayansi. Makala hii inayatalii madai ya pande zote mbili ikitilia mkazo maswali mawili – “Tafsiri na ukalimani ni nini?” na “Je, kutafsiri na kukalimani ni sawa na kurudufu matini chanzi kwa lugha nyingine?” Makala inachunguza ukubalifu wa madai hayo kwa kuyahusisha na nadharia mbalimbali za tafsiri na ukalimani.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X