Main Article Content

Ujitokezaji wa Viambishi Njeo na Athari zake Kifonolojia katika Lugha za Kibantu: Mifano kutoka Lugha ya Shimalila


Pendo Mwashota

Abstract

Makala hii inajadili kuhusu ujitokezaji wa viambishi njeo na athari zake kifonolojia katika lugha za Kibantu. Mifano iliyotumika ni ya lugha ya Shimalila kutoka nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Guthrie (1948), Shimalila ipo katika ukanda wa M 20. Lugha nyingine zilizopo katika ukanda huu ni kama vile Wanda, Mwanga, Kisafwa, Iwa, na Tambo. Kuna vipengele vingi vya kiisimu ambavyo havijafanyiwa uchunguzi katika lugha ya Shimalila. Kwa mfano, vipengele vya kifonolojia, kisintaksia, kimofolojia, kisemantiki na vinginevyo. Pamoja na kuwapo kwa vipengele tajwa kutofanyiwa uchunguzi makala hii inajadili kipengele kimoja cha kimofolojia yaani, viambishi njeo tu. Katika kujadili kipengele hicho cha kiisimu imebainika kuwa lugha ya Shimalila ina ujitokezaji wa pekee wa viambishi njeo vya wakati uliopita tofauti na ilivyo katika lugha ya Kiswahili1. Yaani, katika Shimalila kuna viambishi njeo vya wakati vinavyojitokeza kabla ya mzizi wa shina na vingine vinavyojitokeza baada ya mzizi wa kitenzi. Vilevile Makala inaonesha kuwa wakati mwingine upachikaji wa viambishi njeo katika lugha ya Shimalila huhusisha taaluma ya mofolojia na fonolojia. Chanzo cha data za utafiti huu ni vitabu mbalimbali vinavyohusu lugha ya Shimalila, navyo vimeandikwa na watu mbalimbali wa jamii ya Shimalila ambao malengo yao ni kutafsiri Biblia kutoka katika lugha ya Kiswahili kwenda katika lugha ya Shimalila. Pia, data nyingine zimetokana na hojaji pamoja na usaili wa moja kwa moja wa wazungumzaji watano wa lugha ya Shimalila.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X