Main Article Content

Tafsiri za Riwaya za Kigeni kwa Kiswahili nchini Tanzania


Flavia Aiello Traore

Abstract

Makala hii inazingatia tafsiri ya kifasihi nchini Tanzania enzi za baada ya kujipatia uhuru. Inaeleza baadhi ya mbinu zilizotumiwa na wafasiri wa Kiswahili wakati wakishughulika na kazi za fasihi ya kigeni, hususani jinsi ya kukabiliana na vipengele vya kiutamaduni vya lugha chanzi kama vile kaida za kiutamaduni, misemo, methali n.k. Kwa ajili ya mada hii umechaguliwa mkusanyiko wa tafsiri nne zilizofanywa na Watanzania, yaani Shamba la Wanyama (Fortunatus Kawegere, 1967; tafsiri ya Animal Farm, cha Orwell, 1945), Shujaa Okonkwo (Clement Ndulute, 1973; tafsiri ya Things Fall Apart, cha Achebe, 1958), Mzee na Bahari (Cyprian Tirumanywa, 1980; tafsiri ya The Old Man and the Sea, cha Hemingway, 1952) na Jambo la Maana (Ebrahim Hussein, 1982; tafsiri ya hadithi tatu za Hans Christian Andersen: The Emperor’s New Clothes, 1837, Something, 1858 na The Old Street Lamp, 1847).

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X