Main Article Content

‘Mgogoro’ wa Ushairi wa Kiswahili bado Upo?: Uchunguzi wa Nyimbo za Muziki wa <i>Hip hop</i> na <i>Bongo fleva</i> nchini Tanzania


Shani Omari

Abstract

Nyimbo za muziki wa Hip hop na Bongo fleva zimekuwa maarufu nchini Tanzania kuanzia miaka ya 1980. Nyimbo hizi, kama mojawapo ya tanzu au kipera cha ushairi simulizi wa Kiswahili, zimekuwa ni chanzo kizuri cha utafiti kuhusiana na masuala mbalimbali yahusikayo. Miongoni mwa mambo yanayoonekana kuanza kujitokeza katika nyimbo hizo ni mgogoro wa ushairi kama ule ambao ulitokea miaka ya 1970 katika ushairi wa Kiswahili. Makala hii inalenga kulichunguza suala hili ili kujua namna linavyojitokeza pamoja na mawanda yake. Makala ya utafiti huu imejikita hasa katika kuchunguza mashairi ya nyimbo za muziki huu ili kuchunguza viashiria vya mgogoro huu. Nadharia ya Uhemenitiki ndiyo iliyotumika katika uchambuzi wa data za makala hii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa kuna mjadala wa chini kwa chini unaoendelea baina ya wasanii kupitia nyimbo zao kuhusiana na shairi zuri la muziki wao liweje kifani na hata kimaudhui. Hata hivyo bado ‘mgogoro’ huo haujafikia upeo mkubwa.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X