Main Article Content

Usawiri wa Wahusika wa Kike katika Riwaya Teule za Zainabu Burhani


Rose Mavisi

Abstract

Makala hii inashughulikia usawiri wa wahusika wa kike katika riwaya za Zainabu Burhani. Riwaya hizo ni Mali ya Maskini (1981), Mwisho wa Kosa (1987) na Kipimo cha Mizani (2004). Burhani katika kusawiri wanawake anapiga vita mfumo dume ijapokuwa haepuki athari zake kabisa. Burhani anasawiri vizazi tofauti vya wanawake; kizazi kichanga chenye shime ya kupambana ili kiweze kujikomboa, na kizazi kikongwe kinachokubali hali ilivyo. Nadharia iliyoongoza makala hii ni Unisai wa Kiafrika. Nadharia hii hueleza matatizo yanayowakabili wanawake wa Kiafrika na jinsi wanavyoweza kujiepusha nayo. Kwa mujibu wa nadharia hii Burhani amewasawiri wanawake kwa mtazamo hasi. Jamii nayo pia imewaweka wanawake katika nafasi ya pili baada ya wanaume. Haya yote yanasababishwa na itikadi ya mfumo dume, mazingira na malezi inayowafanya wanawake hawa kuikubali hali yao. Hata hivyo kuna matumaini kupitia kizazi kichanga cha wanawake ambao wanajitahidi kuikata minyororo hii.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X