Historia na Maendeleo ya Kiswahili Nchini Zimbabwe

  • Edwell Dzomba

Abstract

Nchini Zimbabwe Kiswahili kilianza kufundishwa katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe mwezi Agosti, mwaka 2013. Tofauti na nchi za Afrika Mashariki, hadi sasa katika karne hii ya ishirini na moja, Kiswahili hakijaenea sana katika nchi za Kusini mwa Afrika. Kutambulishwa kwa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe ni mojawapo ya ishara za maendeleo ya Kiswahili katika sehemu ya Kusini mwa Afrika. Makala hii inalenga kueleza historia na maendeleo ya Kiswahili nchini Zimbabwe. Lengo kuu ni kuchunguza hali ya Kiswahili nchini Zimbabwe kwa kuangalia maendeleo yake kabla na baada ya kutambulishwa kwa masomo ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe. Hoja yetu kuu ni kwamba, kutambulishwa kwa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe haikuwa chanzo cha kuwapo kwa Kiswahili nchini Zimbabwe. Kiswahili kilikuwa kinatumika katika nyanja mbalimbali lakini ufundishaji ndio ulikuwa haujaanzishwa rasmi. Tumejadili chachu mbalimbali ambazo tunaweza kusema kwamba zinaendelea kusukuma mbele maendeleo ya Kiswahili nchini Zimbabwe, kwa mfano, teknolojia, mavazi, sanaa na biashara, kwa kutaja chache tu. Chachu hizi zimejadiliwa katika kuangalia jinsi zinavyochangia katika kueneza Kiswahili nchini Zimbabwe. Tumehitimisha kwa kuangalia kwamba ni kitu gani kifanyike ili kukikuza Kiswahili nchini Zimbabwe kuwa lugha ya umajumui ya kuwaunganisha Wazimbabwe na watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika nzima kwa ujumla.
Published
2020-02-13
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X