Makosa ya Upatanishi wa Kisarufi katika Ujifunzaji Lugha ya Pili: Mfano wa Wanafunzi wa Kiswahili katika Shule za Upili Wilayani Muhanga, Nchini Rwanda

  • Ntawiyanga Sylvain

Abstract

Makala hii inachunguza makosa ya upatanishi wa kisarufi miongoni mwa wanafunzi wa Kiswahili wa shule za upili wilayani Muhanga, nchini Rwanda. Ingawa kuna miundo kadhaa ya Kiswahili inayofanana na ya Kinyarwanda, wanafunzi Wanyarwanda hutatizwa na tofauti mbalimbali zilizopo kati ya lugha hizo mbili (Ntawiyanga, 2015). Hivyo, lengo kuu la makala hii ni kudhihirisha na kufafanua makosa ya upatanishi wa kisarufi yanayofanywa na wanafunzi Wanyarwanda katika ujifunzaji wao wa lugha ya Kiswahili kwa misingi ya Nadharia ya Uchanganuzi Makosa (Corder, 1967). Kulingana na uchunguzi wa data1 iliyotumika katika makala hii, wanafunzi wengi walifanya makosa mbalimbali katika upatanishi wa kisarufi. Kwa upande mmoja, makosa yaliyofanywa yalitokana na athari za lugha yao ya kwanza ilhali mengine yalitokea pale wanafunzi walipotaka kujumuisha kanuni za lugha ya Kiswahili kwa kujirahisishia ujifunzaji wao. Mapendekezo yanatolewa kwa serikali ya Rwanda, walimu, viongozi wa shule za upili na wadau wa Kiswahili ili waweze kutoa mchango wao katika uboreshaji wa ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili nchini humo.
Published
2020-02-14
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X