Matumizi ya Alama za Kifonetiki za Kimataifa katika Uwasilishaji wa Taarifa za Kimatamshi katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la 3

  • Elither Kindole

Abstract

Kamusi ni kitabu muhimu cha lugha ambacho hutoa taarifa mbalimbali kuhusiana na lugha fulani mahususi. Pamoja na kutoa maana ya neno, kamusi inatakiwa pia kutoa taarifa nyingine muhimu za kisarufi zikiwamo za kimatamshi (Wells, 1985). Uwasilishaji wa taarifa hizi za kimatamshi hutumia alama fulani za kifonetiki zinazowakilisha matamshi hayo. Kwa kutumia Nadharia ya Fonolojia Zalishi, makala hii inachambua Alama za Kifonetiki za Kimataifa (kuanzia sasa AKIKI) zilivyotumika kuwasilisha taarifa za kimatamshi katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2014) toleo la 3 (kuanzia sasa KKS3). Katika uchunguzi huu tunaeleza jinsi AKIKI zilivyotumika. Pia, makala hii inabainisha ubora na udhaifu wa matumizi ya AKIKI katika KKS3. Aidha, mapendekezo ya namna ya kunukuu matamshi kwa kutumia AKIKI yametolewa. Data za makala hii zimekusanywa kwa mbinu ya kusoma kamusi husika kwa umakini. Mbinu hii imetumika kwa kusoma KKS3 ambapo imechunguzwa jinsi taarifa za kimatamshi zilivyowasilishwa ili kubaini AKIKI zilivyotumika.
Published
2020-02-14
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X