Ujenzi wa Maana katika Sitiari na Tashibiha za Kiswahili

  • George J. Kitundu
  • Pendo S. Malangwa

Abstract

Kwa muda mrefu, tamathali za semi zimekuwa zikichunguzwa na kushughulikiwa zaidi katika uwanja wa fasihi kuliko kwenye isimu. Hali hii imewasababishia watu wengi kuwa na dhana kwamba kipengele hiki ni cha kifasihi tu. Kuna ushahidi kwamba zipo tafiti zilizochunguza vipengele hivi katika nyuga za lugha na isimu. Hata hivyo, kuna mitazamo tofauti, hususani katika namna maana za tamathali za semi zinavyojengwa. Mathalani, baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa vipengele vya sitiari na tashibiha vina namna moja ya ujenzi wa maana ilhali wengine wakiamini kuwa vipengele hivi vinatofautiana. Makala hii, kwa kujikita katika uwanja wa semantiki, inadhihirisha kwamba kuna namna maalumu inayotawala ujenzi wa maana katika vipengele vya sitiari na tashibiha. Kila kipengele kina namna yake tofauti ambayo huhusisha mwingiliano wa elementi mbalimbali. Data ya utafiti huu ilikusanywa kutoka katika matini za vitabu na magazeti na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa mwingiliano.
Published
2020-02-14
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X