Makutano kati ya Dini ya Jadi na Dini za Kigeni: Mifano kutoka Riwaya Teule za Kiswahili

  • Lameck E. Mpalanzi

Abstract

Afrika ni bara la watu wanaoamini katika dini ya jadi ama dini za kigeni. Hata hivyo, kwa miongo mingi kumekuwa na tofauti za kiimani kati ya waumini wa dini ya jadi1 na dini za kigeni, kila upande ukijiona uko sahihi kiimani na kimtazamo kuliko upande mwingine. Hali hii imesababisha migongano ya kiitikadi, kinafsia na kijamii. Makala hii inatetea hoja kwamba pamoja na kuwapo kwa migongano hiyo, dini za kigeni ni mwigo na mwendelezo wa misingi iliyowekwa na dini ya jadi ya Kiafrika. Katika kutimiza lengo hili, makala inaeleza dhana ya dini ya jadi na dini za kigeni, mitazamo ya kila dini na makutano ya dini hizo. Data kutoka riwaya teule za kiethnografia inashadidia kuwapo kwa makutano ya dini tajwa. Hoja za ulinganifu na makutano zinaangazia dhana ya kuwapo kwa Mungu, madhabahu, maleba na vifaa vya dini hizo. Hoja zingine zimezingatia malengo ya dini, watendaji wake na suala la utoaji sadaka. Pia, kuna ulinganifu kuhusu miiko, amri, sheria na mitazamo ya dini hizo kuhusu dhana ya maisha.
Published
2020-02-14
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X