Usilimishaji wa Vielelezo katika Fasihi ya Watoto: Mfano kutoka Wasifu wa Mwana Kupona (2008) na Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (2015)

  • Stephen M. Mwendwa
  • Pamela M.Y. Ngugi
  • Catherine Ndungo

Abstract

Makala hii inachunguza usilimishaji1 wa vielelezo vilivyotumika katika hadithi ya Wasifu wa Mwana Kupona (King’ei, 2008) na Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (Hadjavayanis, 2015) na mchango wake katika  kuendeleza ujumbe. Tafiti chache za usilimisho wa vielelezo katika hadithi za watoto zimefanywa (taz. Muthubi, 2005; Kaui, 2011; Sohaimi, 2011; Balodis, 2012; Ratiba, 2014; Omuya, 2017). Hata hivyo, tafiti hizi za awali hazijahusisha moja kwa moja hadithi ya Wasifu wa Mwana Kupona (2008) na Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (2015). Ni katika msingi huu ndipo makala imeshughulikia aina za vielelezo vilivyotumika katika hadithi teule na mchango wake katika kuendeleza ujumbe. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Usilimisho ya George Bluestone (1957) na baadaye ikaendelezwa na Goodman (1976), Andrew (1984) na Starrs (2006). Nadharia ya Usilimisho inahusu uzalishaji wa kazi nyingine huru baada ya kazi ya awali kuzalisha kazi nyingine. Data iliyotumika katika makala hii imetokana na kusoma machapisho mbalimbali maktabani kama vile majarida, tasnifu na vitabu. Vilevile, usomaji, uchambuzi na hata unakili wa vipengele muhimu vinavyohusiana na masilimisho teule ulifanywa. Matokeo ya utafiti yamebainisha kwamba aina za vielelezo vilivyotumika katika hadithi teule ni vibonzo, ramani, picha zilizotiwa rangi na michoro. Aidha, imebainika kuwa vielelezo vinaweza kutumika kupasha ujumbe iwapo vitatumika ipasavyo.

Published
2021-05-04
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X