Main Article Content

Athari za Irabundefu kwenye Maana na Uainishaji wa Maneno yenye Jozi Pambanuzi Finyu katika Lugha ya Kiswahili: Mifano kutoka Kamusi ya <i>Kiswahili Sanifu</i> (TUKI, 2013)


Elishafati J. Ndumiwe

Abstract

Katika lugha ya Kiswahili aina za maneno na maana katika baadhi ya maneno yenye jozi pambanuzi finyu hutofautiana. Utofauti huo unahusishwa na kuwapo kwa irabundefu katika mojawapo ya jozi ya maneno hayo. Kwa hiyo, makala hii inafafanua athari za irabundefu kwenye maana na uainishaji wa maneno yenye jozi pambanuzi finyu katika lugha ya Kiswahili. Data ya makala hii imekusanywa kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya mwaka 2013 kwa kutumia mbinu ya upitiaji wa nyaraka. Aidha, uchambuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Konsonanti-Irabu ya Clements na Keyser (1983). Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba kuwapo kwa irabundefu kunaweza kubadilisha nomino kuwa kitenzi, kitenzi kuwa nomino, kiunganishi kuwa nomino na hata nomino kuwa kivumishi au kibainishi. Vilevile, irabundefu huweza kutofautisha maana katika maneno yenye jozi pambanuzi finyu. Pia, utafiti huu unapendekeza kufanyika kwa tafiti ili kubaini sababu ya utofauti wa maana na kategoria katika maneno ya jozi pambanuzi finyu yenye irabufupi.


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X