Kauli za utendwa/utendewa katika tamthilia za Machozi ya Mwanamke na Heshima Yangu

  • E Mahenge University of Dar es Salaam

Abstract

Kazi hii ni ya utafiti wa kiisimu mitindo unaolenga kulinganisha na kulinganua kazi mbili za tamthiliya za Kiswahili ambazo ni Heshima Yangu (Muhando, 1974) na Machozi ya Mwanamke (Ngozi, 1977). Kwanza, makala inachunguza matumizi ya kauli za utendwa/utendewa katika tamthiliya hizi ili kujua kama ni ya hiari au shinikizo la muktadha. Vilevile lengo ni kujua tofauti ya matumizi hayo kwa waandishi hawa ili kuona wana mwelekeo gani. Pili, makala inatafuta sababu za matumizi haya ya kauli zenye utendwa/utendewa katika tamthiliya hizo. Baada ya hapo, makala inachunguza aina za utendwa/utendewa zilizojitokeza katika tamthiliya hizo. Dai tete linaloongoza makala hii ni kwamba, katika tamthilia hizi mbili, wanaume wanatumia kwa wingi kauli zenye utendwa kuliko wanawake.

Author Biography

E Mahenge, University of Dar es Salaam
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Kiswahili
Published
2010-10-22
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X