Main Article Content

Vionjo vya Riwaya Mpya ya Kiswahili


Said Khamis

Abstract

Neno vionjo linatumika kwa uwili wa maana hapa. Kwanza, hali ya kimajaribio au mwondoko wa utanzu fulani wa fasihi kutoka sura iliyozoeleka kwendea sura mpya inayoanza kujishikashika. Hali ya umajimaji inayotoa sifa bainifu fulani, lakini isiyo na mgando bado, na kwa hivyo kutoweza kuitwa mtindo kwa maana ya trend kwa Kiingereza. Pili, maana ya kuirambisha na kuionyesha hadhira kwa ‘viishira’ kukisia wapi riwaya mpya ya Kiswahili inalekea.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X