Main Article Content

Athari ya Washairi Wakongwe Juu ya Washairi wa Kisasa: Mfano wa Muyaka Bin Haji na Ahmad Nassir


G.K King'ei

Abstract

Kwa kutumia vichwa vya mashairi, umbo na mtindo, msamiati na maudhui, makala hii inavitambulisha baadhi ya vipengele vya usanifu vinavyopatikana katika ushairi wa Muyaka wa Muhaji na jinsi ambavyo vipengele hivyo vimeathiri, kila kimoja kwa kiasi chake, ushairi wa Ahmad Nassir katika diwani ya Malenga wa Mvita. Makala inatumia tungo za Muyaka zilizochambuliwa na Mohamed Hassan Abdulaziz na kuchapishwa mwaka wa 1979. Humu mnaonyesha kiwango cha athari za ushairi wa Muyaka na kuthibitisha jinsi mvuto mkubwa na usanifu wa tungo za Muyaka ulivyowapendeza washairi wa karne ya ishirini kama Ahmad Nassir.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X