Juhudi za Vyombo vya Habari katika Kukuza na Kueneza Kiswahili Nchini Kenya

  • M Kandagor

Abstract

Vyombo vya habari ni asasi muhimu sana katika kukuza na kueneza lugha yoyote ile, hasa katika enzi hii ya utandawazi. Vyombo hivyo ni kama vile idhaa za redio, televisheni na magazeti. Katika nchi ya Kenya kuna vyombo vya habari vinavyotoa huduma anuwai kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya wateja wao. Katika karne hii ya 21, vyombo vya habari vimelazimika kuhakikisha kuwa wateja wao wananufaika kutokana na huduma mbalimbali ambazo hutolewa kila kukicha. Huduma hizo hujumuisha kuwajuza, kuwafundisha, kuwaburudisha na hata kuelimisha jamii kwa namna moja au nyingine. Makala haya yanatathmini juhudi za vyombo vya habari katika kukuza na kueneza Kiswahili nchini Kenya kwa kujikita katika gazeti la Taifa Leo, Idhaa za redio (Citizen na KBC), pamoja na kituo cha runinga1 cha KBC.
Published
2013-07-12
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X