Fantasia Katika Fasihi ya Kiswahili kwa Watoto

  • L Herman

Abstract

Fasihi simulizi na andishi kwa pamoja huchangia sifa moja ya kuwa sanaa ya lugha katika kufikisha ujumbe wake kwa jamii husika. Hii ndiyo ithibati ya sanaa yoyote kuwa fasihi. Kama uwasilishaji wa mawazo katika jamii utafanyika bila kutumia lugha kisanaa basi hapo hakuna fasihi. Katika kutumia lugha na mbinu nyingine za kisanaa katika kufikisha ujumbe kwa jamii, hasa ya watoto, wakati mwingine kuna kuvuka mipaka ya uhalisia kwa kuhusisha wahusika na mambo ya kinjozinjozi au kifantasia kwa makusudi. Mtindo huu wa kutumia fantasia katika kazi za fasihi ni kinyume kabisa na wanataaluma wanaoamini katika ukweli na uhalisia. Wafuasi wa nadharia ya uhalisia wanadai kuwa mwandishi au msanii wa kazi za fasihi anapaswa kuitoa picha ya jamii bila kuidunisha wala kuipigia chuku (Wafula na Njogu, 2007). Swali la kujiuliza hapa ni kuwa, kwa kuwa fantasia inaukimbia ukweli wa uhalisia katika kazi za fasihi hasa kwa watoto, je, mbinu hiyo ina dhima gani kifasihi? Makala haya yana lengo la kushughulikia swali hilo.
Published
2013-07-12
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X