Main Article Content

Mgongano wa matumizi ya lugha mbili Tanzania


Nunuu Abdullah Mohammed

Abstract

Sera ya lugha inaruhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili, lugha za kigeni na lugha za jamii. Fursa hii imewasababishia watu kutumia lugha zote hizo katika sehemu moja kwa wakati mmoja ingawa kila lugha imepangiwa sehemu yake ya matumizi. Hali hii imeleta kero katika matumizi ya lugha hizo. Hivyo, makala haya yamejadili mgongano wa matumzi ya lugha mbili nchini Tanzania pamoja na athari zake. Makala yamedhihirisha kuwa Kiswahili kinapata ushindani mkubwa katika matumizi yake. Aidha, imeonekana kuwa katika matumizi hayo lugha ya Kiswahili na lugha za jamii zimeshushwa hadhi na Kiingereza kimepewa nafasi pana. Ili kuondoa mgongano huo, makala yanapendekeza kuwa sera ya lugha iwekwe kisheria na ijitegemee. Aidha, Kiswahili kitumike katika kufundishia elimu kwa ngazi zote nchini.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886