Main Article Content

Changamoto za Istilahi katika Uandishi wa Tasinifu za Uzamili wa Kiswahili Tanzania


Arnold B. G. Msigwa

Abstract

Uthabiti wa taasisi yoyote ya elimu ya juu hasa katika ngazi ya Chuo Kikuu unatokana na uimara wa programu zitolewazo katika taasisi husika na ubora wa wahitimu katika ngazi husika. Kuimarika kwa programu kama za Umahiri na Uzamivu ni sifa mojawapo ya taasisi ya elimu ya juu. Kuimarika huko hakutawezekana kama eneo la istilahi za kitaaluma zinazotumika katika uwanja husika isimu/fasihi na methodolojia ya utafiti hazitakuwa sanifu na thabiti. Hivyo, makala haya yanafafanua changamoto za kiistilahi katika pragramu za M.A. (Kiswahili) na PhD. (Kiswahili) katika TATAKI kwa uzoefu wa miaka mitano. Swali linaloibuliwa na makala haya ni: je, kutakuwa na usanifu wa programu kama usanifishaji wa istilahi haujafanywa na taasisi husika? Mwito wa makala haya kwa watawala wa TATAKI na Chuo Kikuu kwa ujumla wake, ni kwamba, hima usanifishaji wa istilahi katika Kiswahili hasa katika eneo la methodolojia ufanyike kabla ya jahazi kuzama.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886