Main Article Content

Utayarishaji Wa Vitabu Vya Kufundishia Kiswahili Kama Lugha Ya Kigeni: Haja Ya Kuzingatia Mkabala Wa Mawasiliano


PCK Mtesigwa

Abstract

Makala haya yanakusudia  kutoa misingi muhimu ya utayarishaji wa vitabu vya kufundishia lugha ya Kiswahili kama Lugha ya Kigeni. Kwanza yanataja kwa ufupi malengo ya kujifunza na kufundisha lugha ya kigeni ambayo yanapaswa kuzingatiwa wakati wa kutayarisha vitabu vyenye lengo hilo. Pili, yanataja na kueleza kwa ufupi nadharia na njia mbalimbali za kufundisha lugha ya kigeni. Dhati ya makala haya ni kwamba shabaha kuu ya kufundisha lugha ya kigeni lazima iwe ni kumwezesha mwanafunzi kuijua lugha ya kigeni ipasavyo ili aweze kuwasiliana na watumiaji wenyeji wa lugha hiyo kwa usahihi. Kutokana na shabaha hiyo nadharia ya Mkabala wa Kuzingataia Mawasiliano una nafasi ya pekee, kuliko nadharia nyinginezo, katika kazi ya kutayarisha kitabu cha kufundishia na hata njia zenyewe za kufundisha. Hivyo makala haya yanachambua na kueleza kwa ufupi vipengele muhimu vinavyopaswa kuzingatiwa katika kuandika masomo ya kitabu cha kufundishia kwa kuzingatia Mkabala huo. Kwa upande mmoja vipengele hivyo vitamsaidia mwanafunzi kupata kikamilifu stadi zote muhimu za kuijua lugha na kwa upande wa pili kuyajua mazingira na utamaduni wa lugha ile. Mwishoni makala haya ya inatoa mapendekezo kadhaa kuhusu jinsi ya kukiwezesha kitabu cha aina hiyo kuwa kifaa chenye msaada mkubwa ambao mwanafunzi anaweza kuutumia kwa urahisi kila anapohitaji, mbali na kuwa kisima cha kupatia maarifa yanayotolewa katika kila somo.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886