Main Article Content

Maadili Ya Utafiti


M Mukuthuria

Abstract

Maadili ni kaida zinazoelekeza tabia zetu katika mahusiano yetu ya kila siku na wenzetu (taz. Mathooko na wenzake, 2007:15).  Katika utafiti, maadili ni uwajibikaji na uwelekevu kitabia kuhusu haki za wale wote tunaokutana nao katika utafiti, uwelekevu katika nia na malengo ya utafiti na jinsi ya kutumia matokeo kwa uadilifu ili yaweze kuwa na faida kwa jamii.  Suala hili ni la msingi na ndilo limepewa kipaumbele katika makala hii.  Katika kulishughulikia, tutafafanua ni kwa sababu gani maadili yazingatiwe, wanaotakiwa kuzingatia maadili wakati wa utafiti, tutaangalia ni lini tuanze kuzingatia maadili, masuala ya kimaadili yanayoweza kuibuka na athari za utovu wa maadili katika utafiti; hatimaye, mikondo ya kimkabala au ya kinadharia kuhusu utekelezaji wa maadili uwandani itazingatiwa. 


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886