Matumizi ya nadharia ya umboupeo mawanda katika uchanganuzi wa silabi za Kiswahili

  • Michael A. Mashauri

Abstract

Baadhi ya wataalamu wanaichukulia silabi kama mawanda ambayo kwayo michakato ya kifonolojia hufanyika na au masharti ya mfuatano wa sauti hubainika (taz. Massamba, 2010:189). Katika makala haya tunaonyesha jinsi ambavyo silabi zenyewe pia zinavyokaa katika mawanda silabi yake na kuonyesha jinsi misingi ya nadharia ya Umboupeo Mawanda inavyoweza kutumika kuzichanganulia silabi hizo za lugha ya Kiswahili. Vile vile tunaonyesha mashartizuizi yanayotawala miundo ya silabi za Kiswahili, mpangilio wake na jinsi yanavyoingiliana katika uchanganuzi wa silabi za Kiswahili na katika kufanya tathimini ili kupata muundo wa silabi unaokubalika katika sarufi ya lugha ya Kiswahili. Kwa kuwa nadharia ya Umboupeo Mawanda ni moja kati ya nadharia ndogo ndani ya Nadharia ya Umboupeo, tumetumia misingi mikuu ya nadharia ya Umboupeo isipokuwa tu kipengele kilichoongezeka ni matumizi ya mawanda silabi na ufafanuzi wa mashartizuizi ambao una mtazamo wa nadharia ya Umboupeo Mawanda (Taz. Cassimjee na Kisseberth 1998:4-6). Data zilizotumika ni zile za maktabani na zinazotokana na ujuzi wa lugha ya Kiswahili wa mwandishi.
Published
2017-07-28
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886