Matumizi ya Taifa Leo katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya: nafasi na changamoto

  • James Omari Ontieri

Abstract

Magazeti ni mojawapo ya vyombo vya habari katika jamii vinavyotekeleza jukumu muhimu katika ukuzaji wa lugha. Tunapochunguza magazeti yanayochapishwa kwa Kiswahili, tunagundua kuwa magazeti yanaweza kutoa mchango mkubwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa taaluma ya Kiswahili. Katika mazingira ya Kenya, Taifa Leo ndilo gazeti pekee linalochapishwa kwa Kiswahili na kusambazwa nchini kote. Hali hii inalifanya gazeti hili kuwa nyenzo mwafaka katika ufundishaji wa somo la Kiswahili hususan katika shule za upili nchini Kenya. Kufuatia kutekelezwa kwa mapendekezo ya Tume ya Mackay (1981), Kiswahili ni somo la lazima katika shule za msingi na upili. Makala haya yanalenga kubainisha nafasi ya Taifa Leo katika ufundishaji wa vipengele anuwai vya somo la Kiswahili katika shule za upili. Aidha, changamoto za kutumia gazeti hili katika ufundishaji wa Kiswahili, zinajadiliwa. Data ya makala haya imekusanywa kupitia upekuzi wa maandishi na nakala za gazeti la Taifa Leo kwa kuzingatia vipindi mahususi vya uchapishaji wa gazeti hilo.
Published
2017-07-28
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886