Wahusika wa Kitashtiti katika Gamba la Nyoka

  • Mwenda Mbatiah

Abstract

Makala haya yanachunguza uumbaji wa wahusika katika Gamba la Nyoka ambayo ni mojawapo ya riwaya za Euphrase Kezilahabi. Tumewatambulisha wahusika wakuu watano ambao ni Mambosasa, Mamboleo, Padri Madevu, Mama Tinda na Mzee Chilongo. Hawa ndio wahusika ambao tunawachunguza. Lengo letu ni kudhihirisha kwamba uumbaji wa wahusika hawa umetumia mtindo wa kitashtiti. Mbinu za utunzi zinazohusishwa na tashtiti ni kama vile kinaya, ucheshi, dhihaka na bezo. Kwa vile tashtiti hudhamiriwa kukashifu na pia kupiga vita maovu ya kijamii, makala haya yanaangazia matumizi ya mbinu hizi katika kufanikisha lengo hilo.
Published
2017-07-28
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886