Main Article Content

Uathirianomatini wa Kimtindo katika Ushairi wa Kiswahili: Mfano wa “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona”


Ali H. Chembea
Furaha J. Chai
Rocha M. Chimerah

Abstract

Bakhtin (1981) anaeleza kwamba matini za kifasihi huathiriana na kuhusiana. Kila matini ya kifasihi ina sauti zinazoingiliana na kuhusiana  na matini nyingine zilizopo, zilizopita au zijazo. Hata hivyo, Bakhtin haoni kama ushairi una uathiriano na ushairi mwingine sawia kama  inavyojitokeza katika riwaya. Baadhi ya wataalamu waliohakiki “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona” wanadai kuwa tenzi hizi  zimeathiriana. Makala hii inalenga kudhihirisha uathirianomatini wa kimtindo kati ya “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona”  katika ushairi wa Kiswahili. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Usemezano ya Bakhtin. Ingawa, kwa mujibu wa nadharia hiyo, riwaya  ndio utanzu unaotegemea zaidi uathiriano na matini nyingine kuliko ushairi, makala hii inapanua mawanda yake kwa kuchunguza  uathiriano wa kimtindo katika ushairi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwapo kwa uathiriano wa muundo, msamiati, majibizano na   tamathali za semi.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886