Kiswahili
https://www.ajol.info/index.php/ksh
Kiswahili is an interdisciplinary international journal devoted to the study of Kiswahili language, linguistics and literature. Its main aim is to gather and disseminate under a single cover a wide variety of research and discussion of fundamental concern to all those scholars who have an interest in Kiswahili language, linguistics and literature.en-USCopyright is owned by the journal.massamba45@gmail.com (D.P.B. Massamba)iks@udsm.ac.tz (F.N. Joster (Associate Editor/Mhariri Msaidizi))Mon, 31 Mar 2025 17:20:37 +0000OJS 3.3.0.11http://blogs.law.harvard.edu/tech/rss60MASIKIDU kama Miviga ya Kuchochea Maendeleo ya Kiswahili
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292087

Makala hii inachunguza namna Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani – MASIKIDU yanavyoweza kutumiwa kama nyenzo ya kukuza maarifa ya Kiswahili ndani na nje ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, eneo ambalo sehemu kubwa ya wakazi wake wanaweza kuwasiliana kwa Kiswahili. Maadhimisho haya, yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 7 Julai, huwakutanisha wadau mbalimbali wa Kiswahili ambao hujadiliana masuala kadha wa kadha kuhusu lugha ya Kiswahili na utamaduni wake. Kwa hiyo, katika maadhimisho haya, wadau wanaweza kukumbushana na kupeana majukumu ya kuendeleza Kiswahili. Katika makala hii, MASIKIDU yamejadiliwa kama tukio linalochangia kubadilishana maarifa, fikra na mitazamo kuhusu lugha na fasihi ya Kiswahili. Kwa kutumia kiunzi cha miviga ya mpito chenye hatua tatu, yaani (i) mtengo, (ii) mabadiliko, na (iii) ujumuikaji, makala hii inafafanua namna MASIKIDU yanavyoweza kukuza maarifa ya washiriki na kusambaza maarifa hayo kwa wengine. Kwa ujumla, ikiwa kila mdau atashiriki katika MASIKIDU kwa dhamira ya dhati, kuna uwezekano wa maadhimisho haya kuwa kioo muhimu kwa wanagenzi na wanazuoni wa Kiswahili duniani.
Angelus Mnenuka
Copyright (c) 2025
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292087Mon, 31 Mar 2025 00:00:00 +0000Kukua kwa Matumizi ya Kiswahili Duniani na Utamaduni wake*
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292088

Makala hii iliwasilishwa tarehe 7 Julai 2023 mjini Copenhagen, Denmaki kuhusu maendeleo ya Kiswahili duniani. Makala inaeleza historia ya Kiswahili kwa muhtasari kwa kubainisha jamii za Waswahili, yaani wenyeji wa ukanda wa pwani wa Afrika Mashariki. Aidha, makala imetaja taasisi mbalimbali zilizoanzishwa kwa ajili ya kukuza Kiswahili. Kiswahili kinafundishwa katika taasisi mbalimbali katika maeneo mbalimbali duniani. Mwandishi amedokeza pia ukrioli wa utamaduni wa Kiswahili kwa kubainisha athari za mila mbalimbali katika Kiswahili, zikiwamo tasnia za sheria, kilimo, biashara na matibabu. Mwisho, mwandishi amedokeza msamiati wa Kiswahili kutoka katika lugha mbalimbali za Kiafrika na nje ya bara la Afrika, kutoka Ulaya na Asia.
Abdulaziz Yusuf Lodhi
Copyright (c) 2025
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292088Mon, 31 Mar 2025 00:00:00 +0000Ufinyaji wa Fursa za Kiswahili Nchini Tanzania: Uchunguzi Kifani wa Sera ya Lugha na Mpangolugha
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292090

Mpangolugha nchini Tanzania huipa lugha ya Kiingereza hadhi ya juu, Kiswahili hadhi ya kati na lugha za kijamii hadhi ya chini (Msanjila, 2009; Rugemalira, 2013; Ndumiwe, 2019; Kawonga, 2023). Lugha iliyopewa hadhi ya juu hutumika katika shughuli rasmi kama vile mahakama za juu, diplomasia, mikataba na shughuli za kimataifa. Fursa katika lugha hutegemea mawanda mapana ya matumizi ya lugha inayobidhaishwa. Hata hivyo, lugha ya Kiswahili nchini Tanzania imepewa mawanda finyu katika shughuli rasmi ikilinganishwa na lugha ya Kiingereza. Kwa hiyo, utafiti huu unachunguza namna mpangolugha na sera ya lugha vinavyofinya fursa za Kiswahili nchini Tanzania. Data za makala hii zimekusanywa maktabani na uwandani. Kwa upande wa maktabani, data zilikusanywa kutoka andiko la Sera ya Utamaduni (WEU, 1997) kwa kutumia mbinu ya usomaji wa matini. Aidha, kwa upande wa uwandani, data zilikusanywa kutoka kwa wahitimu wa ualimu katika Kiswahili, wafasiri, wakalimani na walimu wa shule za sekondari kwa kutumia mbinu ya usaili. Nadharia ya Ikolojia ya Kiisimu iliyoasisiwa na Wendel (2005) ilitumika katika kuchanganua data za utafiti huu. Utafiti huu umebaini kuwa mpangolugha na sera ya lugha huminya fursa katika Kiswahili kama vile tafsiri, ukalimani, ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni, uhariri na uchapishaji katika Kiswahili. Utafiti huu unapendekeza kuandaliwa kwa sera ya lugha na mpangolugha mpya ili kuiweka lugha ya Kiswahili katika darajia la juu. Suala hilo litaongeza fursa za kiuchumi katika lugha ya Kiswahili.
Elishafati J. Ndumiwe, Elishafati J. Ndumiwe
Copyright (c) 2025
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292090Mon, 31 Mar 2025 00:00:00 +0000Impediments to the Development of Kiswahili in the Education Sector in Uganda
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292092

This study explores the challenges facing the growth of the Kiswahili language in the Ugandan education system. Despite noticeable efforts by the government, the development of Kiswahili through the education system still faces various obstacles. Data was collected from policymakers, coordinators, and language policy implementers, who were purposively selected. Data was analysed using a qualitative approach. Based on a thematic analysis of data, it was established that the growth and development of the Kiswahili language in Uganda, through the education system is still low. This is due to a lack of political will, the absence of effective strategies for implementing language policy regarding Kiswahili, the non-deployment of available Kiswahili teachers, and the inadequacy of materials and resources for teaching and learning Kiswahili. Similarly, ethnolinguistic rivalries have derailed efforts towards Kiswahili development in the education sector. Suggested practical strategies to address these challenges include: strong political will, adequate supply of Kiswahili teaching materials, as well as recruitment and deployment of more Kiswahili teachers. Additionally, tackling negative attitudes and conducting further research on language perceptions will enhance its acceptance and development. These findings are important for policymakers in guiding the formulation of necessary policies that will impact Kiswahili teaching and usage in Uganda.
Innocent Agume, Nathan Oyori Ogechi, David Majariwa
Copyright (c) 2025
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292092Mon, 31 Mar 2025 00:00:00 +0000Kiswahili na Uandishi, Uchapishaji na Usomaji Nchini Tanzania
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292126

Makala inaangazia fursa zilizopo katika uandishi na uchapishaji kwa Kiswahili nchini Tanzania, na kuhoji kwa nini mwandishi na mchapishaji hafaidiki kikamilifu na fursa hizo. Ukosefu wa tija katika shughuli hizo umesababisha mdororo mkubwa katika tasnia ya uchapishaji ambayo inajumuisha uandishi, utoaji vitabu, usambazaji na usomaji, na kuwalazimisha waandishi kuacha kuandika, kuacha kuchapisha kazi zao, au kujitafutia mbinu mbadala za kutoa na kusambaza kazi zao. Makala inaeleza kuwa kuzorota kwa usomaji nchini Tanzania ni chanzo kikuu, na pia ni matokeo, ya mdororo huo. Inaelezwa kuwa ufumbuzi wa tatizo hili sharti uanzie katika kutambua uhusiano na mwingiliano uliopo kati ya tasnia ya vitabu, sera ya elimu na mitaala ya lugha. Inasisitizwa kuwa msingi wa maendeleo ya tasnia ya uchapishaji katika mfumo wa ubepari tulio nao ni usomaji; bila kuwa na hadhira pevu ya wasomaji haiwezekani kuwa na tasnia hai ya vitabu. Mitaala ya sasa haiweki uzito katika usomaji; haitambui kwamba, ili kuwa na taifa la wasomaji, usomaji sharti uanzie katika ngazi ya chini kabisa katika shule za elimu ya awali na kuendelezwa hadi shule za msingi na sekondari ili hatimaye litengenezwe taifa la watu wenye tabia na utamaduni wa kusoma. Watu hao ndio watakaokuwa wateja (yaani soko) wa mwandishi na mchapishaji, na ndio watakaoibeba tasnia ya vitabu. Ili kukipata kizazi hicho kipya cha wasomaji, mapendekezo yanatolewa kuhusiana na utoaji wa motisha kwa waandishi, uboreshaji wa mitaala, maktaba za shule na za umma, na uwekezaji katika utoaji na ununuzi wa vitabu vya ziada na ridhaa kwa upande wa serikali na asasi binafsi.
Mugyabuso M. Mulokozi
Copyright (c) 2025
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292126Mon, 31 Mar 2025 00:00:00 +0000Mchango wa Kiswahili katika Kuleta Amani kwa Maendeleo Endelevu Barani Afrika
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292127

Lengo la makala hii ni kueleza mchango wa lugha ya Kiswahili katika kuleta amani barani Afrika kwa ustawi wa maendeleo endelevu. Data zilikusanywa kwa njia ya mapitio ya nyaraka na zilichambuliwa kwa njia ya uchambuzi wa maudhui. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba Kiswahili kina mchango katika kuleta amani barani Afrika kwa maendeleo endelevu kwani kinarahisisha mawasiliano na kuunganisha jamii za Kiafrika. Pia, Kiswahili kinawaunganisha watu wa makabila na itikadi tofauti na kuleta ushirikiano na maelewano miongoni mwao. Vilevile, Kiswahili kinatumika kama nyenzo ya kusuluhisha migogoro inayojitokeza katika jamii barani Afrika kutokana na ukabila kwani hakifungamani na kabila lolote. Hivyo, Kiswahili ni miongoni mwa tunu muhimu zinazotakiwa kuthaminiwa na jamii za Kiafrika kwa maendeleo endelevu.
Tumaini Mahendeka
Copyright (c) 2025
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292127Mon, 31 Mar 2025 00:00:00 +0000Uzoefu wa Ufundishaji na Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili nchini Uganda
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292128

Suala la ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili nchini Uganda limewashughulisha watalaamu mbalimbali (Kahaika, 2018; Kahaika, 2020; Jjingo, 2020). Wataalamu hao wanadai kuwa Kiswahili ni lugha ya kigeni nchini Uganda hasa kwa kuzingatia matumizi yake finyu katika jamii. Licha ya watalaamu hao kukiri hivyo, bado haijaeleweka namna lugha ya Kiswahili inavyofundishwa nchini Uganda hususani kwa kuzingatia mbinu zitumikazo. Hivyo, makala hii inabainisha namna lugha ya Kiswahili inavyofundishwa nchini huko kwa kuelezea mbinu mbalimbali zinazotumiwa katika ufundishaji na ujifunzaji wake katika ngazi tofautitofauti na changamoto zinazolikumba zoezi zima la ufundishaji na ujifunzaji wa lugha hiyo. Vivyo hivyo, makala hii inafafanua namna lugha ya Kiswahili ilivyofanikiwa nchini Uganda kwa kubainisha nyanja mbalimbali ambako lugha hiyo inatumika. Pia, ili lugha ya Kiswahili ienee zaidi nchini Uganda, makala hii imetoa mapendekezo ambayo yakizingatiwa yatasaidia katika shughuli mbalimbali za ueneaji wa Lugha hiyo. Aidha, makala hii iliongozwa na Nadharia ya Upangaji wa Lugha ya Haugen (1983) inayosisitiza uteuzi wa lugha kisheria na pia utekelezaji wake kupitia shughuli mbalimbali. Data za makala hii zilipatikana kwa kufanya udurusu wa nyaraka mbalimbali zinazopatikana maktabani na mtandaoni pamoja na uzoefu wa mwandishi alionao katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchini Uganda.
Racheal Munyakiire
Copyright (c) 2025
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292128Mon, 31 Mar 2025 00:00:00 +0000Uzoefu wa Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili nchini Ghana
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292129

Makaka hii inalenga kufafanua kuhusu uzoefu wa ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili nchini Ghana. Kwa miaka mingi, suala la uzoefu wa ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili nchini Ghana halijafafanuliwa na wanaisimu ama walimu wa Kiswahili. Makaka hii, kwa kuongozwa na Nadharia ya Isimujamii (Trudgill, 1983; Hudson, 1985; Mekacha, 2000; Msanjila, Kihore na Massamba, 2011) inajadili uzoefu wa ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, mwandishi alitumia uzoefu wake kwa kuwa alikuwa mwanafunzi wa Kiswahili nchini Ghana kwa miaka mitano na kufundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni kwa miaka mitatu nchini Ghana na katika nchi za nje aliweza kujadili uzoefu wa ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili nchini Ghana. Makala hii inajadili historia ya Kiswahili, ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika taasisi mbalimbali hasa za elimu, changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili nchini Ghana. Pia, makala hii inatoa mapendekezo kuhusu namna ya kukuza Kiswahili nchini Ghana na duniani kote.
Joshua Agbozo
Copyright (c) 2025
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292129Mon, 31 Mar 2025 00:00:00 +0000Maendeleo ya Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe 2013-2024
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292134

Kiswahili kilianza kufundishwa katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe mwezi Agosti, mwaka 2013. Ni miaka kumi na mmoja sasa tangu Kiswahili kianzishwe katika chuo hicho. Makala hii inachunguza maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe. Data za utafiti zilikusanywa kupitia majadiliano ya kundi lengwa na walimu wanaofundisha Kiswahili, upitiaji wa matini hususani zile za sera za lugha katika elimu na usaili wa viongozi wa chuo hususani wakuu wa idara za vitivo vya Chuo Kikuu cha Zimbabwe. Lengo kuu lilikuwa kuchunguza utekelezaji wa sera ya lugha katika elimu ya kufundisha Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe, maendeleo, changamoto, mahitaji na matarajio. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, ingawa Kiswahili kilianzishwa miaka kumi na mmoja iliyopita, bado kuna mambo mengi yanayotakiwa kufanywa ili kustawisha ufundishaji na ujifunzaji wake. Walimu wa Kiswahili ni wachache kuliko idadi ya wanafunzi, vifaa vya kufundishia ni vichache, muda wa kusoma ni mchache na Kiswahili hakisomwi kama digrii. Makala hii imetumia njia saba za utekelezaji wa sera za lugha katika elimu za Kaplan na Baldauf (1997, 2003) kama kiunzi cha nadharia katika kuchunguza maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe.
Edwell Dzomba, Lillian Mazvita Munetsi
Copyright (c) 2025
https://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/292134Mon, 31 Mar 2025 00:00:00 +0000