Main Article Content

Matumizi ya Anagramu, Kanuni ya Rebasi, Seti, Emoji na Akronimi kama Mitindo ya Sanaa ya Uandishi


Benard Odoyo Okal

Abstract

Sanaa ya uandishi imeendelea kutokea katika mfumo wa kikabari, kihiroglifu, kilogografu, kisilabi, na kialfabeti. Imebainika kuwa tunapoendelea kimaandishi kutoka mfumo mmoja tunaelekea kuhama pia na vipashio vingine vya mifumo ya awali. Hivyo basi, chembechembe za mifumo ya awali zingali zinadhihirika katika mitindo mingine ya kisasa ya matumizi ya lugha kama tunavyoona katika rebasi, seti, na emoji. Kwa hiyo, makala haya yanalenga kufafanua mitindo ya rebasi, seti na emoji, pamoja na anagramu na akronimi kama sanaa ya uandishi ili kutambua ishara zinazotumiwa na zilizokubaliwa katika lugha. Makala yanahusisha dhana, dhima, historia, na maendeleo ya sanaa ya uandishi. Yanaonyesha pia jinsi mitindo ya anagramu, rebasi, seti, emoji, na akronimi inavyodhihirika kama sanaa ya uandishi. Data zilikusanywa maktabani kwa kutumia upekuzi, kuteuliwa kidhamirifu na kuchanganuliwa kimaudhui.


The art of writing has systematically developed from cuneiform, hieroglyphic, logographic, syllabic to alphabetic writing. However, it has emerged that as we develop writing from one system to the other we also tend to carry along some aspects of the earlier systems. Hence, some elements of the early writing systems tend to be present even in the current writing systems as witnessed in the use of rebus, set and emoji. This article, therefore, intends to explain how the rebus, set, emoji, and also anagram and acronym styles are used as forms of writing in language. The article involves the concept, functions, history and development of art of writing in its scope. It also shows how anagram, rebus, set, emoji and acronym styles manifest themselves as forms of writing. Data was collected by the use of observation from the library, purposively sampled and analysed thematically.


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2164