Main Article Content

Hali ya taaluma ya ukalimani Tanzania: jana, leo na kesho


Titus Mpemba

Abstract

Umuhimu wa ukalimani katika mawasiliano umeongezeka kutokana na utandawazi. Utandawazi umerahisisha kukutanika na kuwasiliana kwa watu wazungumzao lugha tofauti kupitia wakalimani. Kutokana na ongezeko hilo la umuhimu wa ukalimani, kumekuwa na jitihada mbalimbali katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanaandaliwa wataalamu wa kutosha kuendana na ongezeko hilo. Hivyo, kumekuwa na ongezeko la tafiti katika uwanja huu na taasisi mbalimbali zimeanzishwa ili kuandaa wataalamu wa fani hiyo na baadhi ya asasi zilizokuwapo zimepanua mafunzo yake na kujumuisha programu za uzamili. Mathalani, mpaka kufikia mwaka 2011, Barani Ulaya peke yake kulikuwa na takribani programu za mafunzo ya ukalimani kwa “ngazi ya umahiri zipatazo 135” (Munday, 2008: 6). Mapinduzi haya, pamoja na kuendeshwa kwa makongamano mbalimbali na kuchapishwa kwa machapisho mbalimbali kutokana na juhudi hizi, yameuwezesha ukalimani kujichomoza na kusimama kama taaluma mahususi inayojitegemea (Garzone & Viezzi, 2002: 11). Kwa kutumia mkabala wa kihistoria, makala haya yanachunguza jinsi nchi ya Tanzania ilivyoitikia jitihada hizi za kukuza ukalimani na kufanya hivyo yatatathmini mafanikio, mbinu na changamoto za jana na leo na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kufanikisha harakati hizi hapo kesho. Makala yanalenga kujibu maswali makuu matatu: (1) Ukalimani kama somo, ulianza kufunzwa lini nchini Tanzania? (2) Hivi sasa taaluma ya ukalimani ina hali gani? na (3) Nini mustakabali wa taaluma ya ukalimani nchini Tanzania?

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886