Main Article Content

Ruwaza ya Simulizi za Watumwa katika Riwaya ya <i>Uhuru wa Watumwa</i>


Grace Henry

Abstract

Makala haya yanachambua ruwaza ya simulizi za watumwa inavyojitokeza katika riwaya ya Uhuru wa Watumwa (1934). Uhuru wa Watumwa ni riwaya iliyotafitiwa na kuchambuliwa na wataalamu mbalimbali kwa namna tofautitofauti. Kwa mfano, Mohamed (1974), Senkoro (1974, 1976), Mlacha (1985, 1991) na Mulokozi (2000) wanachambua vipengele vya kifani na kimaudhui vya riwaya hii kama vile jina la kitabu, muundo, mtindo na dhamira za riwaya hii. Senkoro (1976) na Mulokozi (2000) wanadai kuwa hii ni riwaya ya kwanza ya Kiswahili. Pamoja na hayo, Mulokozi (2003) anabainisha kuwa riwaya hii ni simulizi ya watumwa. Simulizi za watumwa kama uwanja unaojitegemea zinaunganishwa na mambo mbalimbali kama vile ruwaza, motifu na maudhui. Pamoja na kuunganishwa na mambo hayo, makala haya yanaweka wazi ujitokezaji wa kipengele kimoja tu cha ruwaza ya simulizi za watumwa namna kinavyojitokeza katika riwaya ya Uhuru wa Watumwa.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886