Main Article Content

Tathmini ya Mitaala ya Ufundishaji wa Kiswahili Ngazi ya Sekondari katika Matumizi ya Nadharia nchini Tanzania


Hamad Khamis Juma

Abstract

Makala haya yanalenga kutathmini mitaala ya ufundishaji wa Kiswahili ngazi ya sekondari katika matumizi ya nadharia nchini Tanzania. Ili kufikia lengo hilo, makala haya yamegawanywa katika sehemu kuu nne. Sehemu ya kwanza ni utangulizi ambao unafasili na kufafanua dhana ya mtaala, mitaala ya ufundishaji na maudhui ya muhtasari wa Kiswahili katika shule za sekondari. Sehemu ya pili, inafafanua dhana za nadharia, nadharia za ufundishaji na mikabala ya kinadharia iliyotumika katika makala haya. Sehemu ya tatu ambayo ndiyo kiini cha makala haya inajadili matumizi ya nadharia katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule za sekondari. Pia, inajadili ufundishaji wa msamiati kwa kuhusisha mikabala ya kinadharia ya mwingiliano na mawasiliano pamoja na kutathmini kufaa kwa matumizi ya nadharia katika mitaala ya ufundishaji wa Kiswahili katika shule za sekondari, changamoto na mapendekezo ya utatuzi. Sehemu ya nne ni hitimisho ambalo linaelezea kwa muhutasari matokeo ya uchunguzi wa makala haya.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886