PROMOTING ACCESS TO AFRICAN RESEARCH

Kiswahili

The AJOL site is currently undergoing a major upgrade, and there will temporarily be some restrictions to the available functionality.
-- Users will not be able to register or log in during this period.
-- Full text (PDF) downloads of Open Access journal articles will be available as always.
-- Full text (PDF) downloads of subscription based journal articles will NOT be available
We apologise for any inconvenience caused. Please check back soon, as we will revert to usual policy as soon as possible.

DOWNLOAD FULL TEXT Open Access  DOWNLOAD FULL TEXT Subscription or Fee Access

Usawiri wa Mwanamke Mchawi katika Riwaya za Kiethnografia za Kiswahili

Lameck Mpalanzi

Abstract


Usawiri wa mwanamke katika fasihi umechunguzwa na wanazuoni  mbalimbali. Tafiti zilizopo zinamuonesha mwanamke kama mzazi, chombo cha kuzalisha mali, chombo cha anasa, mtu asiye na uhuru na/ama mfanyakazi wa nyumbani. Kwa upande mwingine, tafiti chache  zinachunguza mwanamke kwa jicho la kianthropolojia na kifalsafa. Kwa mfano, Mekacha (1993) anamlinganisha mwanamke sawa na ibilisi/shetani kwa kuwa anatazamwa kama chanzo cha maovu yote. Naye, Mesaki (1993) anachunguza namna mwanamke anavyobeba tajiriba za kichawi katika jamii nchini. Anaona kuwa wanawake vikongwe wanauawa zaidi kutokana na tuhuma za uchawi. Mwandishi wa makala hii anachochewa na fikra za Mekacha (khj) na Mesaki (khj) na hatimaye anachunguza namna uchawi wa mwanamke unavyojitokeza katika riwaya za kiethnografia za Kiswahili. Makala hii inalenga uchambuzi wa riwaya nne za kiethnografia za Kiswahili. Makala inabainisha kuwa ijapokuwa wanawake na wanaume wanaweza kuwa wachawi, wanawake wana mamlaka zaidi katika magenge ya wachawi. Kadhalika, wanawake ndiyo wateja wakuu, washirika wakuu, washauri na wahanga katika masuala yanayohusu uchawi. Aidha, mambo yanayowafanya wanawake kujihusisha na uchawi ni changamoto za kisaikolojia, kijinsia na kiontolojia.

Full Text:


No subscription journal articles available during site upgrade.AJOL African Journals Online