Main Article Content

‘Ukiushi Juu ya Ukiushi’-Mchomozo wa Kifonolojia katika Mashairi ya E. Kezilahabi: Mifano kutoka Diwani ya <i>Dhifa</i>


E. Dzomba
A.K. Mutembei

Abstract

Ushairi wa Kiswahili umechunguzwa na wataalamu kadha kwa kutumia mikabala mbalimbali kama vile muundo, lugha, taswira au mkabala wa kiishara, nahata maumbo. Mkabala wa makala hii unaendeleza mjadala kwa kuegemea katika elimu-mitindo. Mkabala wa kielimu-mitindo katika ushairi umewahi kushughulikiwa na wanazuoni mbalimbali waliochunguza mchomozo katika ngazi mbalimbali za kielimu-mitindo kama fonolojia, mofolojia na sintaksia. Dhana ya mchomozo katika tafiti hizi imechunguzwa kwa kuangalia ukiushi wa kaida na marudiorudio ya vipengele fulani katika uwasilishaji wa dhamira mbalimbali katika ushairi. Ushairi wa Kiswahili wa wanausasa umejadiliwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni ushairi unaokiuka kaida zilizozoeleka za utungaji wa mashairi ya Kiswahili. Hata hivyo, kuna mchomozo ambao tafiti zilizotangulia hazikuutilia mkazo katika kuangalia suala la ukiushi. Kwa kutumia Mkabala wa Kielimu-mitindo, makala hii inachambua kimya kama mchomozo wa kifonolojia katika diwani ya Euphrase Kezilahabi, Dhifa (2008). Mashairi haya, kupitia matumizi ya kimya, yanabeba sifa za kipekee ambazo zinatofautiana na sifa za mashairi mengine ya wanausasa. Kwa hiyo, kimya katika mashairi haya kimejadiliwa kama kipengele kinachoonesha ‘ukiushi juu ya ukiushi’ katika ushairi wa Kezilahabi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha vipengele kama ridhimu, onomatopea, takriri, asonansi na konsonansi kama vijenzi vya mchomozo wa kifonolojia.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886