Main Article Content

<i>Al-Inkishafi</i>: Wahusika wa Uhalisiajabu katika Kuendeleza Maudhui ya Dini ya Kiislamu


Ali Hamisi Chembea

Abstract

Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu Utenzi wa Al-Inkishafi. Kwa mfano, Hitchens (1972), Allen (1977), Mlamali (1980), Momanyi (1991), Mulokozi (1999) na Mberia (2015). Kwa kipindi kirefu, mijadala ya kihalisiajabu  imeangaziwa zaidi katika utunzi na uhakiki wa kazi za kinathari. Uhalisiajabu haujachunguzwa katika uchambuzi wa kazi za kishairi labda kutokana na mtazamo finyu kuwa utanzu huo hauna mawanda mapana ya kimaudhui na kimtindo. Hata hivyo, baadhi ya tenzi za Kiswahili, hususan tenzi kongwe za Kiswahili zimejikita kikamilifu katika uhalisiajabu. Ingawaje ushairi huwasilishwa kwa njia ya mkato, uketo wake wa maudhui katika jamii ya Waswahili ni kadhia pana sawia na ilivyo katika tanzu nyingine za fasihi. Utafiti huu, pamoja na kuweka wazi kwamba uhalisiajabu unadhihirika katika ushairi wa Kiswahili, umethibitisha ufaafu wa mtazamo huu katika kuchanganua maudhui ya dini. Makala hii imechanganua wahusika wa kihalisiajabu katika Utenzi wa Al-Inkishafi na kudhihirisha namna wanavyoendeleza maudhui ya dini ya Kiislamu.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886