Main Article Content

Nathari Butu: Utanzu Mpya wa Fasihi?


Ahmad Kipacha

Abstract

Makala haya ni pendekezo la fikra mtambuka kuhusu aina mpya ya utanzu wa fasihi andishi ya Kiswahili wa nathari butu. Kwa sasa hakuna makubaliano miongoni mwa wananadharia wa fasihi ya Kiswahili juu ya idadi za tanzu za fasihi za Kiswahili. Kwa ujumla, tanzu zinazobainishwa ni ushairi, tamthilia, riwaya, hadithi fupi, novella na insha za kifasihi. Kiumbo, hakuna umushkeli katika uanishaji wa tanzu za ushairi na tamthilia. Utata upo katika kundi au kumbo la kinathari linalojumuisha tanzu za riwaya, hadithi fupi, novella na insha za kifasihi. Makala haya yanaweka bayana chanzo cha utata huo na kupendekeza suluhisho la mjadala juu ya kumbo la nathari zenye ubunilifu na zile zenye ukweli mtupu. Pendekezo linajengwa katika makala haya juu ya vigezo vya kuzingatiwa katika uainishaji wa nathari halisi zenye sifa za ufasihi tuziitazo nathari butu (creative nonfiction). Tunapendekeza fikra juu ya utanzu mahususi wa “nathari butu” kama aina mpya ya utanzu wa fasihi andishi ya Kiswahili wenye sifa pambanuzi za kiuanishaji.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886